Utafiti wa Kiolezo cha Mtazamo wa LGBTQI+ cha F&M Global Barometers 2026
Karibu kwenye Utafiti wa 2026 wa Haki za Kibinadamu wa F&M Global Barometers wa Kiolezo cha Mitazamo ya Watu wa LGBTQI+!
Utafiti huu unalenga watu wanaojitambulisha kuwa LGBTQI+, ikiwemo mwanamke anayevutiwa kimapenzi na wanawake wengine, mwanaume anayevutiwa kimapenzi na wanaume wengine, mtu anayevutiwa kimapenzi na jinsia yake, mtu anayevutiwa kimapenzi na jinsia zote mbili, transjenda, mtu anayejitambua na jinsia tofauti na ile aliyozaliwa nayo na/au mtu mwenye jinsia mbili, miongoni mwa wengine. Utafiti huu utachukua takribani dakika 2–5 kukamilika. Majibu yote ya utafiti huu yatatunzwa kwa usiri kamili na hayatabainisha utambulisho wako, kwa kuzingatia viwango vya juu vya kimataifa vya utafiti.
Sisi, F&M Global Barometers, tunakuomba utafakari kuhusu uzoefu wako wa haki za kibinadamu kama mtu wa LGBTQI+ katika nchi yako. Majibu yako yatatusaidia kuelewa mabadiliko ya haki za kibinadamu za watu wa LGBTQI+ duniani kote kadiri muda unavyopita. Tafadhali tuma maswali au hoja zako kwa Dkt. Susan Dicklitch-Nelson, Mtafiti Mkuu wa F&M Global Barometers, kupitia gbgr@fandm.edu.
Utafiti wetu umekaguliwa na kuidhinishwa na Bodi ya Ukaguzi wa Utafiti ya Franklin & Marshall College (IRB). Maelezo kuhusu ridhaa yenye ufahamu yanapatikana HAPA. Maswali kuhusu haki zako kama mshiriki wa utafiti huu yanaweza kuelekezwa kwa Mwenyekiti wa sasa wa IRB kupitia irb@fandm.edu.